Tanzania

Kampeni za Injili: Maeneo Sita Dar Es Salaam

Pamoja na timu ya Wainjilisti na Viongozi wa kuabudu wenye vipawa. Mwinjilisti Daniel Kolenda atakuwa akiyatembelea maeneo SITA ndani ya Dar Es Salaam,Tanzania mwezi wa Kumi 2021: Gongo la Mboto, Jangwani, Kawe, Kigamboni, Kimara na Mbagala.

Ikiwa unaweza kuhisi kuna kitu kinakosekana moyoni na nafsini mwako, hapa ndipo mahali unapostahili kuwepo. Njoo kwenye Mikutano Mikubwa ya Injili ya CfaN, upokee baraka zako, na umkaribishe Yesu maishani mwako.

Hakuna kiingilio chochote katika kuhudhuria Mikutano yetu Mikubwa ya Injili, kwa hiyo waalike marafiki zako, familia na kila mtu anayehitaji kusikia Habari Njema za Yesu Kristo!

screen

Gongo la Mboto

6 – 10 Octoba

Je, ungependa kupokea habari kuhusu ule mkutano wa injili utakaofanyika katika mji huu? Tafadhali, Jisajili hapa.

Jisajili

Jangwani

6 – 10 Octoba

Je, ungependa kupokea habari kuhusu ule mkutano wa injili utakaofanyika katika mji huu? Tafadhali, Jisajili hapa.

Jisajili

Kawe

6 – 10 Octoba

Je, ungependa kupokea habari kuhusu ule mkutano wa injili utakaofanyika katika mji huu? Tafadhali, Jisajili hapa.

Jisajili

Kigamboni

6 – 10 Octoba

Je, ungependa kupokea habari kuhusu ule mkutano wa injili utakaofanyika katika mji huu? Tafadhali, Jisajili hapa.

Jisajili

Mbagala

6 – 10 Octoba

Je, ungependa kupokea habari kuhusu ule mkutano wa injili utakaofanyika katika mji huu? Tafadhali, Jisajili hapa.

Jisajili

Kimara

6 – 10 Octoba

Je, ungependa kupokea habari kuhusu ule mkutano wa injili utakaofanyika katika mji huu? Tafadhali, Jisajili hapa.

Jisajili

Shuhuda za Uponyaji

Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, na viziwi wanasikia.

image

16 Februari 2020

WARRI, NIGERIA

Ulemavu mkubwa wa macho uliosababishwa na kufifia kwa mboni za macho na kuwa na ugonywa wa mtoto wa jicho katika macho yote mawili uliponywa kabisa! Mungu alimfanya aone tena.

image

15 Februari 2020

WARRI, NIGERIA

Aliekuwa kiziwi katika sikio lake la kushoto tangu kuzaliwa kwake, na sasa anaweza kusikia! Mungu ni yuleyule, jana, leo na milele. Anataka kuyafungua macho yako!

image

14 Februari 2020

WARRI, NIGERIA

Aliyekuwa kiziwi katika sikio lake la kushoto naye kwasasa amepona kabisa.

image

19-22 Novemba 2020

Singida, Tanzania

Mwanaume mwenye tatizo la mguu kwa miezi mitatu apokea uponyaji siku ya pili ya mkutano.Anasema alikuwa akisikia kama moto unawaka kwenye mguu wake, alikuwa na maumivu makali sana na hakuweza kutembea kabla ya mkutano.Usiku wa leo ameruka jukwaani akiwa hana maumivu tena!

image

12-15 Novemba 2020

Tabora, Tanzania

Binti aliyekuwa na maumivu kwenye tumbo lake kwa miezi 18 aliponywa kabisa.

Christ for all Nations (CfaN)

Shirika la Christ for all Nations lilianzishwa na Mwinjilisti Reinhard Bonnke mwaka 1974 baada ya kuhudumu kwa miaka michache akifanya kazi kama mmisionari aliyezuru Afrika mara kwa mara. Shauku yake kubwa ya kuona mataifa yakiokolewa ilitokana na mfululizo wa maono ambapo aliona bara zima la Afrika likiwa limeoshwa kwa damu ya Yesu na kusikia sauti ya Roho Mtakatifu moyoni mwake ikimnong'onezea maneno haya mara nyingi “Afrika itaokolewa!”. Hali hii ilimfanya achukue hatua katika imani akiwa pamoja na timu ndogo sana na kuanzisha huduma hii ya uinjilisti Afrika – “kutoka Cape Town hadi Cairo.”

Mrithi wa Bonnke, Mwinjilisti Daniel Kolenda anahudumu kama Rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Christ for all Nations, na chini ya uongozi wake, CfaN haliendelei tu kuihubiri Injili bali pia limejitoa kikamilifu kutumia kila aina ya teknolojia na fursa anazotupa Mungu kwa ajili ya kazi kuu ya kuvuna nafsi.

Daniel anaiongoza huduma ya CfaN kuendelea mbele kwa kazi ya upako katika lengo letu kuu la kuihubiri injili ulimwenguni kote kwa kutumia mkakati, wa makusudi na kwa uzito.

Baada ya miaka mingi ya ajabu ya wokovu, uponyaji, ukombozi na umiminaji wa Roho Mtakatifu, timu ya CfaN ikiongozwa na Daniel Kolenda, inaanza kuzifikia nchi nyingi mpya katika bara la Afrika kama njia ya kuitikia wito wa makanisa kutaka kusaidiwa.

icon

Hii si bahati mabaya

UPENDO WA DHATI utanena na moyo wako!

image

Kuna kusudi linalofanya kazi maishani mwako sasa hivi zaidi ya chochote unachoweza kufikiria, kukijua na hata kukihisi. Ni kana kwamba ulimwengu wenyewe unajaribu kukutumia ujumbe. Umekuwa ukitafuta ishara. Basi ishara yenyewendio hii.

Pakua gazeti hili na uuruhusu ujumbe wa Mwana Mpotevu ukuguse. Ikiwa uko tayari kurudi nyumbani na kumpokea Yesu maishani mwako, wasiliana nasi kwa kujaza fomu iliyo hapa chini nasi tutawasiliana nawe.

Ndiyo, naomba nitumiwe gazeti hili la bure la mtandaoni!

AFRIKA ITAOKOLEWA

Mkutano wa mwisho wa Injili Tanzania 2021

553,000

Mahudhurio

60,752

Kadi za Waliookoka

1,500+

Makanisa yaliyoshiriki

person

Daniel Kolenda ni mwinjilisti wa kisasa na mhubiri wa kimataifa anayesifika. Amewaleta zaidi ya watu milioni 22 kwa Kristo ana kwa ana kupitia mikutano mikubwa ya nje ya injili katika baadhi ya sehemu hatari zaidi, ngumu na za mbali sana duniani.

Kama mrithi wa Reinhard Bonnke ambaye ni mwinjilisti maarufu ulimwenguni , Daniel ni rais na Afisa Mkuu Mtendaji wa Christ for All Nations; huduma ambayo imeandaa baadhi ya mikutano mikubwa zaidi ya injili katika historia ya dunia.

Daniel ni mhubiri wa kizazi cha tano mwenye kipawa na ambaye huduma yake inaambatana na upako mkubwa wa kiinjili na miujiza ya ajabu inayofuata mfano wa Yesu; kuhubiri, kufundisha na kuponya. Vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, na viziwi wanasikia — hata amewahi kushuhudia wafu wakifufuliwa — lakini cha muhimu zaidi, maskini wanahubiriwa Injili. Msisitizo wa nia moja wa Injili ndio unaoifanya huduma ya Daniel Kolenda na Christ for all Nations kuwa ya kipekee sana.